Rais Samia: Pengo la Membe halizibiki

Rais Samia: Pengo la Membe halizibiki

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema pengo aliloacha mwanasiasa mbobezi Bernard Membe haliwezi kuzibika.
Rais Samia ameyasema hayo leo Mei 14,2023 akitoa salamu za rambirambi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Amesema, katika vitu mwanadamu hawezi kuzuia ni siku ya kufa na siku ya kuzaliwa.

“Hata kama Dk atapanga operesheni siku ya kuja kwako, kama Mungu hajapanga uzaliwe basi kitatokea chochote tu na operesheni haitafanyika.” Amesema Rais Samia na kuongeza

“Sote  tumepokea kwa uzuni na mshtuko mkubwa baada ya kuugua kwa muda mfupi.
“Tunaungana na watanzania wote kutoa pole kwa mjane wa marehemu na watoto Cecilia, Richard na Denis.
“Kifo cha Membe kimewashtusha wengi ndani na nje ya nchi kwani alikua mashuhur, msiba huu si wenu familia peke yenu, serikali tupo pamoja kwa hakika nguzo kuu imepotea.”Amesema
Amesema, binafsi alikua na Membe kwenye nyakati tofauti katika medali za siasa, alikua mchapakazi, kifo chake kimeacha pengo si tu kwa taifa lake hata kwa mataifa aliyoyatumikia.
“Tumekuja dunia kwa ridhaa yake na tutaondoka kwa ridhaa yake, maamuzi ya Mungu ayalaumiwi, tunapaswa kushukuru.” Amesema Rais Samia.
Membe amefariki dunia juzi katika hospitali ya Kairuki kutokana na tatizo la mfumo wa upumuaji, anatarajiwa kuzikwa kesho kutwa Mei 16,2023 Rondo Chiponda mkoani Lindi

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x