Rais Samia: Tuungane kupambana na vita ya uchumi

NCHI za Afrika zimetakiwa kukabiliana na vita ya uchumi iliyopo hivi sasa duniani,

Hayo yamesemwa leo Septemba 23, 2022 na Rais Samia Suluhu akihutubia katika kongamano la 12 la Chama cha Ukombozi cha Frelimo nchini Msumbiji.

Rais Samia amesema Tanzania, Msumbiji na nchi nyingine za Afrika hazipo katika vita ya ukombozi kwani kama ni Uhuru zilishapata, vita pekee ambayo wanapaswa kupambana nayo kwa sasa ni ya kiuchumi.

“Mapambano ya uhuru wa kiuchumi siyo mepesi, tunahitaji kuwa pamoja kama tulivyopambana dhidi ya ukoloni.” Amesema na kuongeza

“Tunaposema ‘Aluta Continua’ yaani mapambano bado yanaendelea ni mapambano halisi na lazima yaendelee ili kuinua uchumi wa nchi zetu na uwezo wa kifedha wa vyama vyetu ili vitekeleze majukumu yake vizuri.”

Amesema ili kutimiza lengo hilo, vijana wa nchi hizo wanapaswa kufunzwa kupitia Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Habari Zifananazo

Back to top button