Rais Samia – ‘twendeni tukahesabiwe’

RAIS Samia Suluhu Hassan amelihutubia taifa akiwataka wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la kitaifa linalotarajiwa kuanza mapema kesho Agosti 23.

Rais Samia amesema katika matukio kama hayo kipindi cha nyuma sensa ilikuwa ikifanyika kila Jumapili ya mwisho ya Agosti, hata hivyo kutokana na sababu za kidini kwa baadhi ya wananchi kuwa kanisani serikali imeona ifanye zoezi hilo siku ya Jumanne ambapo pia itakuwa siku ya mapumziko.

“Sensa inatokea mara moja tu kila baada ya miaka 10. Sensa zilizopita zimefanyika 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Kabla ya uhuru, Tanzania Bara wakati huo ikitambulika kama Tanganyika ilifanya sensa tano na sensa ya kwanza ilifanyika 1913, 1921, 1931, 1948, na 1957. Kwa upande wa Zanzibar sensa ilifanywa mara moja tu mwaka 1958 wakati wa ukoloni na utawala wa sultani.

Sensa hizi zilikosa vigezo vya kisanyansi na zilifanyika kwa malengo mahusisi ya watawala wa kati huo ambayo ilikuwa kujua idadi ya manamba, wanaoweza kwenda vitani na malengo mengine. Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 itakuwa ya sita kufanyika tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1964.

Niwakumbushe wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa kwenye zoezi hili litakalo anza kesho tarehe Agosti 23, amesema Rais Samia katika hotuba yake.

Habari Zifananazo

Back to top button