Rais Senegal atangaza ukomo wake

RAIS wa Senegal, Macky Sall amesema April 2, mwaka huu atafikia ukomo wa nafasi yake ila hafahamu ni lini uchaguzi mpya utafanyika.

Sall amesema haiwezekani uchaguzi wa rais mpya kuanza kabla ya wakati huo. Alisema tarehe ya uchaguzi itategemea mdahalo wa kitaifa uliopangwa kuanza Jumatatu, ambao unajumuisha mashirika ya kiraia, vyama vya siasa na wagombea.

“Tarehe 2 Aprili 2024 nafasi yangu kama mkuu wa Senegal itakamilika. Ningependa mjadala huu utatuliwe kwa uwazi.” Amesema Sall.

Advertisement

Tangazo lake linaondoa hofu kwamba alikuwa akipanga kuongeza muda wake, huku kukiwa na mzozo wa kisiasa.
Sall amekuwa chini ya shinikizo la kutangaza tarehe ya uchaguzi tangu kujaribu kuuchelewesha mapema mwezi huu.