Rais wa Iran afariki dunia

TEHRAN, Iran: RAIS wa Iran, Ebrahim Raisi amefariki dunia katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Iran kufuatia ajali ya helikopta iliyotokea hapo jana.

Asubuhi ya leo Ikulu ya nchi hiyo imethibitisha kifo cha rais huyo na kueleza kwamba katika helikopta hiyo, Raisi aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amirabdollahian, Gavana wa Mashariki ya Azerbaijan, walinzi wa rais na maafisa kadhaa. Taarifa hizo zinaeleza kwamba hakuna uwezekano wa watu hao pia kuwa hai.

Vikosi vya uokozi vikiwa Mashariki mwa Jimbo la Tehra, nchini Iran kufanya uokozi wa ajali ya helikopta iliyochukua maisha ya Rais wa Iran na viongozi wengine waandamizi wa taifa hilo.

“Ndege ya Rais yote imeteketea kwa moto katika ajali hiyo hivyo hakuna uwezekano wa waliokuwemo ndani ya ndege hiyo kuwa hai, wote wanahisiwa kufa” Kimeeleza kituo kimoja maarufu cha habari maarufu nchini humo.

Rais wa huyo amefariki akiwa na miaka 63 alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa awamu ya pili mwaka 2021.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7Lg0iVul9I/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Makamu wa kwanza wa Rais wa nchi hiyo Mohammad Mokhber anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo na anatakiwa aitishe uchaguzi mpya wa rais ndani ya siku 50.

Habari Zifananazo

Back to top button