Rais wa zamani China afariki

#BREAKING #NEWS: Rais wa zamani wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin, ambaye aliongoza nchi kupitia mabadiliko kisiasa mwishoni mwa mwaka 1980 amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 96, Xinhua imeripoti.

Jiang aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China kuanzia 1989 mpaka 2002 alichukua madaraka kutoka kwa Zhao Ziyang na kuliongoza taifa hilo lenye watu wengi zaidi duniani.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati ya Kudumu ya Bunge la Kitaifa la Watu wa Jamhuri ya Watu wa China (PRC), Baraza la Jimbo la PRC, Kamati ya Kitaifa ya Watu wa China. Mkutano wa Ushauri wa Kisiasa, na Tume Kuu za Kijeshi za CPC na PRC.

Habari Zifananazo

Back to top button