Rashford mchezaji bora Februari

MKALI wa mabao wa Manchester United, Marcus Rashord amechaguliwa na chama cha soka ‘THE FA’ kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England kwa mwezi Februari.

Ndani ya mwezi huo, Rashford amecheza michezo minne na kufunga mabao matano, wakati timu yake ikishinda michezo mitatu.

Tuzo hiyo ni ya tatu kwa Rashford, alitwaa mwezi September, Januari na Februari.

Kocha wa timu hiyo Eric Ten Hag ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari kwa mara ya pili, alishinda tuzo hiyo mwezi September.

Habari Zifananazo

Back to top button