Rashford nje wiki kadhaa

NYOTA wa Man United, Marcus Rashford atakosa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla kesho na mechi zingine za EPL kutokana na maumivu ya misuli.

Rashford mwenye mabao 28 msimu huu katika michuano yote, aliumia katika mchezo dhidi ya Everton Jumamosi na kutolewa nje dakika 80.

Man United itakutana na Sevilla baada ya hapo itarejea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Notts Forest Jumamosi wiki hii kesha itarudiana na Sevilla nchini Hispania wiki ijayo.

Hata hivyo kukosekana kwake kunatoa nafasi kwa wachezaji wengine wa nafasi yake, akiwemo Jadon Sancho, Elanga au Anthony Martial kama tu kocha Eric Ten Hag ataendelea kumtumia Wout Weghorst kama mshambuliaji wa mwisho.

Habari Zifananazo

Back to top button