BAYERN MUNCHEN imekamilisha uhamisho wa mkopo wa beki Mreno, Joao Cancelo kutoka Manchester City.
Mkataba huo ni mkopo wa awali wenye kipingele cha kumnunua kwa zaidi ya £61m (€70m).
Cancelo amechapisha ujumbe wa kuwaaga Man Cit`y kwenye ukurasa wake wa Instagram “Ukiwa Mwananchi siku zote ni Mwananchi, asanteni sana.”
Ruben Dias, Ederson na nyota wa Arsenal aliyewahi kuitumikia City, Oleksandr Zinchenko ni miongoni mwa waliotuma jumbe zao za kwaheri.