SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa ratiba ya michezo ya Ngao ya Jamii itakayochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kuanzia August 9, 2023.
Ratiba hiyo inaonesha mchezo wa kwanza kesho Agosti 9,2023 utakuwa kati ya Yanga dhidi ya Azam FC.
Mchezo wa pili Agosti 10, 2023 Simba dhidi Singida.
Mshind wa mchezo wa kwanza atakutana na mshindi wa mchezo wa pili kumpata bingwa. Na akayepoteza mchezo wa kwanza atakutana na atakayepoteza mchezo wa pili.