Rayvany: Muziki nje umenipa heshima

MSANII wa Bongo fleva, Raymond Shaban, ‘Rayvanny’ amesema safari yake  ya ughaibuni imeendelea kumpa heshima na kusababisha jina lake kuwa kubwa na kufanya kupokewa kwa heshima nchini Uingereza na Ufaransa

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa shukrani zake kwa wote wanaomuunga mkono

“Napenda ninachokiona. Upendo na heshima kwa jina langu iko katika kiwango kingine kabisa. Shukrani kubwa kwa wabunifu wote na makampuni makubwa ya Paris (Wiki ya Mitindo), shukrani kubwa kwa vyombo vyote vya habari nchini Uingereza na Ufaransa”

Advertisement

“Lakini pia, shukrani kwa marafiki zangu/waimbaji, tulikuwa na nyakati nzuri tukitumia muda pamoja studio. Kwa mashabiki wangu duniani kote, nataka kuwajulisha tu kwamba nakuja kwenu”.ameandika Rayvanny