MFANYABIASHARA maarufu na mwanasiasa mkongwe visiwani Zanzibar Mohamed Raza amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam ambako alikua akipatiwa matibabu.
Raza ambae amewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja atazikwa leo saa 11 jioni katika makaburi ya Kisutu.
Mmoja wa wanafamilia Ibrahim Raza amethibitisha kifo cha mfanyabiashara uyo ambae Mei 9,2023 Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi alifika jijini Dar es Salaam kumjulia hali.