RC Arusha aagiza kuanza ujenzi shule wasichana

ARUSHA; Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ameagiza kuanza mara moja kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya masomo ya sayansi inayojengwa wilayani Longid,o baada ya kuonekana hali ya kusuasua kwa mradi huo licha ya serikali kutoa Sh bilioni 3.

Pia ameagiza umeme na maji yawe yamefika haraka katika eneo hil, ili kuwezesha ujenzi huo uliopo nje ya muda kuanza na Desemba mwaka huu shule huyo iwe imeshakamilika.

Mongella ametoa agizo hilo wilayani Longido, mara baada ya kutembelea eneo hilo na kubaini changamoto kadhaa.

Advertisement

3 comments

Comments are closed.