RC Arusha aiagiza halmashauri kujenga vibanda vya biashara

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Stephen Ulaya kujenga vibanda vya biashara badala ya kuwaachia wananchi au wazabuni wajenge hali itakayoleta sintofahamu ya ulipaji wa kodi baadaye.

RC Mongella ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha baraza maalum la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wilayani Longido kwa mwaka 2021/22.

Amesema endapo halmashauri hiyo ikiwaachia wananchi au wazabuni wajenge vibanda vya biashara eneo hilo hapo baadaye kutaibuka utata wa ulipaji kodi na kupelekea halmashauri hiyo kukosa mapato kwasababu wafanyabiashara watavipangisha kwa fedha kubwa kisha kulipa halmashauri hela ndogo za mapato.

“Msiwape wazabuni wajenge maduka hapa mtaleta mgogogoro baina ya halmashauri na wafanyabiashara na hii tabia kwa Jiji la Arusha imewakuta sana sasa isije kutokea hapa, mkakosa mapato kwa kukusanya kodi ndogo na Julai mosi, mwaka huu nakuja mwenyewe kuizindua na nikija nakagua vyoo na miundimbinu mingine muhimu”

  1. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido amesema stendi hiyo ya mabasi ambayo haijaanza imetumia Sh milioni 25 ambapo menejimenti imetenga fedha za kukamilisha miundimbinu ya choo, kuweka kifusi, taa na mageti.

Diwani wa Kata ya Longido, Thomas Ngobei amesema uwepo wa stendi hiyo utawezesha wilaya hiyo kupata mapato mengi zaidi na kutoa ushauri kwa mkurugenzi Ulaya kuhakikisha huduma zote za muhimu ndani ya stendi hiyo ziwepo ili kuwezesha ushuru kukusanywa na kutoa angalizo ushuru huo ukusanywe na watu sahihi ili ili kuepusha migongano ya kimaslahi.

Habari Zifananazo

Back to top button