MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewataka wakandarasi wanaopewa kazi mbalimbali mkoani humo kuhakisha wanatimiza kazi zao kwa mujibu wa mikataba, ili wasikwamishe miradi.
Mongella alitoa agizo hilo jana katika hafla ya kusaini mikataba awamu ya pili katika mwaka wa fedha 2022/23.
Amewataka wakandarasi waliosaini mikataba hiyo, kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo, ili kuhakikisha maendeleo yanakua kwa kasi kutokana na miundombinu ya barabara.
Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh bilioni 18.235 kwa ajili ya kujenga barabara za Arusha, kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).
Amesema Rais Samia hana deni la barabara na Mkoa wa Arusha, ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mijini na vijijini, hivyo Tarura wahakikishe wanasimamia vizuri barabara hizo.