MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewashauri Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), kuboresha huduma zao na kuzitoa kwa gharama nafuu, ili wadau wa serikali, taasisi na idara zake waifanye kuwa kimbilio la kwanza katika matengenezo ya magari na huduma zingine.
Pia ameipongeza Temesa kwa kuja na mbinu mpya ya kujali wateja na kutatua changamoto zilizokuwepo awali, kwani magari ukitengeneza vyema watu watakukimbilia.
Mongella ametoa rai hiyo leo jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa kikao Cha Temesa na wadau wake na kuongeza kuwa huduma zikiboreshwa hakuna mdau atakukimbilia mtaani, badala yake atakimbilia Temesa.
“Miaka ya nyuma kulikua na changamoto tofauti na sasa, kuna maboresho makubwa, lakini endeleeni kuboresha, ili tuifanye kimbilio letu la kwanza, maana ukipata huduma bora hutakimbilia mtaani,” amesema.
Naye Mtendaji Mkuu wa Temesa, Lazaro Kilahala, amesema hiyo ni taasisi wezeshi yenye kutoa huduma kwa serikali kuleta ufanisi zaidi.