RC awatunuku vyeti polisi Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewatunuku vyeti na zawadi askari polisi wa mkoa huo waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi mwaka 2022.

Hafla ya utoaji wa zawadi imefanyika Februari 08, 2023 katika Uwanja wa FFU Mbeya ikitanguliwa na Paredi lililoandaliwa kwa ajili ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza baada ya kukagua na kutoa vyeti na zawadi kwa askari, Juma Homera amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kuimarisha ulinzi na usalama hali inayopelekea kupungua kwa uhalifu.

Mkuu wa mkoa huyo amewataka askari wa Jeshi la Polisi kupendana, kuacha kufanyiana
matendo mabaya ambayo yatapelekea kushusha morali ya utendaji kazi na kuchafua taswira ya jeshi la polisi.

Homera amewataka maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kudumisha nidhamu katika utendaji kazi za kila siku ili kujiepusha na vitendo vya rushwa nk.

Aidha amewapongeza askari waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi za Polisi ikiwa ni pamoja na kukamata silaha, kupambana na majambazi. Pia amewapongeza wadau wa Jeshi la Polisi na kuwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano ili kufikia malengo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Jumla ya askari 43, mtumishi raia 01 na wadau werevu 14 wametunukiwa vyeti na zaidi
mbalimbali katika hafla hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button