TANGA: MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, ameripoti Leo kwenye kituo chake kipya cha kazi na ametaja vipaumbele 14 vitakavyomuongoza katika utumishi wake mkoani humo.
Amevitaja vipaumbele hivyo katika hafla ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanal Evance Mtambi amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuboresha kiwango cha ufaulu katika elimu , kuboresha huduma za afya.
“Katika kilimo tunakwenda kuleta tija katika mazao ya katani,Korosho na viungo yaweze kuwa mkombozi kwa mkulima lakini kuongeza kiwango Cha mapato “amesema Mkuu wa mkoa huyo.
Pia Dk Batilda amevitaja vipaumbele vingine ni miradi ya kimkakati na ubunifu wa fursa zinazotokana na miradi hiyo, ulinzi na usalama wa watu na mali zao, udhibiti wa mfumko wa bei hasa kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhani.
Haya hivyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman amesema kuwa mabadiliko ya uongozi yanayofanywa na Rais Samia yamelenga katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kiutendaji .
Nae Katibu wa wakuu wa Wilaya za Tanga Zainab Abdallah amesema kuwa wao kama MADC wamejipanga katika kusimamia malengo makuu manne ambayo ni kusimamia miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato,kusikiliza na kutatua kero za wananchi lakini na ubunifu katika kuzifikia fursa za kiuchumi zilizopo kwenye wilaya zao.