RC Geita apiga marufuku michango bila kibali

MKUU wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amepiga marufuku watendaji wa vijiji na kata kuendesha michango ya miradi kwa wananchi pasipo kibali cha Mkuu wa Wilaya na watakaoikuka utaratibu watachukuliwa hatua.

Shigella ametoa maagizo hayo wakati akizungumuza katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Lulembela, kata ya Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya kupokea malalamiko ya kutoka kwa wananchi.

Ameeleza kushangazwa na uwepo wa michango lukuki wanayotozwa wakazi wa kijiji cha Lulembela kwa ajili ya miradi mbalimbali ya elimu ambapo michango hiyo imepelekea kuibua taharuki na migogoro kijijini hapo.

Amesema, serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa pesa za elimu bure kila mwezi na pesa za miradi mbalimbali na mwezi Mei mwaka huu mkoa umepokea Sh bilioni 9.

7 ya mradi wa elimu wa Boost hivo michango iwe ya uwazi.

Ameagiza michango itakayopitishwa na ofisi ya mkuu wa wilaya, wananchi wasomewe mapato na matumizi na kisha karatasi za mchanganuo zibandikwe kwenye mbao za matangazo kuepusha taharuki isiyokuwa ya lazima.

“Yakifanyika hayo bila kufuata utaratibu ninaosema wananchi kataeni kutoa, kwa sababu michango hiyo ni batili haijazingatia utaratibu, kwa sababu haiwezekani kila tukija hapa na sisi tunaonekana tumekula hela.”

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Sakina Mohamed amesema, kupitia mradi wa Boost, wilaya imepokea Sh bilioni 1.9 huku kata ya Lulembela pekee imetengewa kiasi cha Sh milioni 959 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lulembela, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Lulembela, Frank Goryo ameeleza michango iliyoendelea kwa sasa kijijini hapo inahusiana na malipo ya fidia ya maeneo zinapojengwa shule mpya.

Habari Zifananazo

Back to top button