RC Geita ataka nidhamu fedha za maji

RC Geita, Martin Shigella

MKUU wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, amewataka Wakala wa MajiSafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuzingatia nidhamu katika matumizi na usimamizi wa fedha za bajeti na mapato ya miradi ya maji.

Shigella ametoa maelekezo hayo wakati akizungumuza na watumishi wa Ruwasa katika kikao maalum cha tathimini ya utendaji kwa watumishi wa wakala wa maji mkoani hapa.

Amesema nidhamu na weledi katika fedha na miradi ya maji itawezesha mkoa kufikia malengo uliyowekewa kwa mjibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Advertisement

“Mwaka jana tulikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 10 zilizoletwa kwenye halmashauri zetu, tukajitahidi kufanya vizuri, mwaka huu bajeti imepanda mpaka Sh bilioni 12 kwa hiyo ni fedha nyingi sana.

“Malengo yetu ya Ilani ya CCM ni kufikia asilimia 85 ifikapo 2025 kwa ameneo ya vijijini, kwa sasa hivi tupo asilimia 66, na kwa mjini lengo ni kufikia asilimia 90, lakini sasa hivi tupo asilimia 72.

“Tunayo miaka mitatu tu, kwa hiyo tukijipanga vizuri maji vijijini tutakuwa tumeyafikia malengo ambayo yameelekezwa na ilani ya CCM kwa silimia 85 vijijini na kwa mjini kufikia asilimia 90,” amesema.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *