RC Kagera aonya wanaotoa vibali raia wa kigeni

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwasa amesema serikali mkoani humo inaendelea na uchunguzi kwa viongozi mbalimbali ikiwemo vikosi vya ulinzi na usalama juu ya taarifa za kutoa vibali na vitambulisho ya taifa kwa raia wa kigeni ili waishe kama wazawa.

RC Mwasa amesema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa katika kambi ya Jeshi ya Kaboya Kikosi cha 21 ambapo ameshiriki dua na sara ya kuwaombea marehemu 619 walioshiriki kupigana vita ya Kagera na Uganda mwaka 1978/1979 na kuzikwa katika kambi hiyo.

Advertisement

Alisema kuwa Mashujaa wote walikuwa wazalendo wa nchi yao lakini sasa hivi serikali imebaini baadhi ya watumishi wasio waadilifu ambao wameshiriki kugawa vitambulisho vya taifa pamoja na kutoa vibari kiholela kwa wananchi kutoka nchi jirani kuja kuishi nchini kama wazaliwa wa nchi hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Alisema kuwa uchunguzi ukikamilika mtumishi yoyote atakayebainika na tuhuma hizo asitegemee kuhamishwa kituo kingine cha kazi au kukimbilia sehemu nyingine isipokuwa atavuliwa vyeo vyake na sheria kuchukua mkondo wake.

Amesikitishwa na watu wasio waadilifu na wazalendo ambao wamekosa kulinda mipaka yao mpaka kuuza nchi yao kwa raia wa kigeni wanaoweza kuchochea mvurugano wa amani kwa wakati wowote.

“Ili uwe shujaa sio lazima upigane Vita,uwezi kuwa shujaa wakati unapokea Rushwa na kutoa vibali vya watu kuishi nchini mwako wakati ni wageni unauza haki ya wazawa ,leo tunawaombea maelfu marehemu waliongoza vikosi vya mapigano ya kivita  na kupoteza maisha katika kuwapogania Watanzania ,walioilinda nchi yao, lakini wakati huo kuwa watu wachache wanapoteza uzalendo na kuuza nchi yao sitakubari Kama mkuu wa mkoa tunamalizia uchunguzi tutawachukulia hatua kali “alisema Mwasa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *