RC Katavi ataka umeme vituo vya afya, shuleni

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Katavi limepewa hadi Julai 30,2023 kuhakikisha majengo yote ya vituo vya afya, hospitali za wilaya, shule za msingi na sekondari yanaunganishiwa umeme, ili kazi ziweze kufanyika kwa ufanisi katika maeneo hayo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipotembelea na kukagua kituo cha Afya Kazima kilichopo Kata ya Kazima, Manispaa ya Mpanda.

Advertisement

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho, Mganga mfawidhi kituo cha Afya Kazima Dk. Herman Kimango, amesema licha ya kituo hicho kuanza kutoa huduma Juni 19, 2023 bado umeme ni changamoto katika eneo hilo.

RC Mrindoko ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Kazima na maeneo jirani kukitumia Kituo cha Afya Kazima, kwani tayari kimeanza kutoa huduma baada ya ujenzi wake ulioanza Julai 20, 2022 kwa gharama ya Sh milioni 250 kukamilika.

Ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa usimamizi mzuri wa fedha zilizotolewana serikali kutoka katika tozo za miamala ya simu, kwani kituo hicho kimejengwa katika viwango vinavyotakiwa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *