RC Makala awasha pampu ya maji Kigamboni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala akiwasha pampu ya kusukuma maji kutoka kwenye Visima vya Maji Kimbiji na Mpela

WAKAZI wa Wilaya ya Ilala, Kigamboni na Temeke mbioni kusahau mgao wa maji baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala leo Oktoba 28, 2022 kuwasha pampu ya kusukuma maji kutoka kwenye Visima vya Maji Kimbiji na Mpela kuelekea kwenye tanki la kupokea na kusambaza maji.

Kuwashwa kwa pampu hiyo itapunguza makali ya mgao wa maji unaoendelea katika jiji la Dar es Salama na Pwani kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na Wilaya ya Ilala yote ikiwemo katikati ya jiji kuanzia Jumanne Novemba Mosi.

Advertisement

Makalla amesema visima hivyo vinazalisha Lita Milioni 450 kwa saa na maji yanayozalishwa yanapelekwa kwenye tanki lenye uwezo wa kupokea Lita Milioni 15.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa maji uliopo, Makalla ameielekeza Dawasa kuhakikisha Wakandarasi wanafanya kazi usiku na mchana ili ifikapo Jumanne Lita Milioni 70 ziwe zimefika kwa wananchi.

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Davis Mwamunyange aliishukuru serikali kuiwezesha Dawasa kukabiliana na changamoto iliyopo hivi sasa.

“Hata Roma haikujengwa siku moja, Dar es Salaam wakazi wanaongezeka Dawasa tunajitaidi kwa kadri ya uwezo wetu kuhakikisha maji ya uhakika yanapatika, mradi huu wa Kigamboni utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa maji.”Amesema

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mpaka sasa visima saba kati ya 12 vya Kimbiji na Mpela vimekamilika na vile ambavyo havijakamilika vipo hatua za mwisho.

Amesema mradi huo unagharimu shilingi bilioni 23.5 ambazo zimetolewa na serikali unalenga kusambaza huduma yam aji kwa wakato wapatao 250,000.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *