RC Malima aipiga tafu Pamba FC

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima anaamini timu ya Pamba inayoshiriki ligi ya ‘Championship’ bado ina nafasi ya kupanda ligi kuu .

Malima amesema hayo leo alipozunguza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo.

Malima amesema kuwa timu hiyo imeonyesha uwezo mkubwa katika michezo yao hivyo ina uwezo wa kucheza ligi kuu kikubwa wachezaji waongezee  bidii.

“Sina shaka na nyie uwezo wenu nimeuona uwanjani naamini benchi la ufundi litafanyia marekebisho eneo la umaliziaji ili muweze kufunga magoli mengi ” amesema Malima

Katika hatua nyingine Malima amewasii viongozi pamoja na timu kwa ujumla kufanya maandalizi mazuri ili waweze kushinda mchezo ujao wa mchujo dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma Mei 21 mwaka huu ili kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Mei 28  kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza

Amewakabidhi wachezaji wa Pamba kiasi cha Sh milioni 3 ambapo ahadi yake ilikuwa Sh milioni 1na Sh milioni mbili kutoka kwa Jambo food products.

Kwa upande wake naodha wa timu hiyo Jerry Tegete amesema pamoja na kukosa nafasi ya kupanda moja kwa moja kwa hivi sasa wamejielekeza kufanya vyema katika mchezo wa mchujo dhidi ya Mashujaa fc ili wakazi wa Mwanza wapate kuiona timu yao ikiwa ligi kuu kwa msimu ujao.

Timu ya Pamba FC imemaliza michezo ya ligi hiyo kwa msimu huu ikiwa nafasi ya tatu mbele ya Kitayose fc ya na Jkt Tanzania ambazo zimepata nafasi ya kupanda ligi kuu moja kwa moja hivyo timu ya Pamba itacheza mchezo wa mchujo dhidi ya Mashuja fc ya Kigoma iliyomaliza nafasi ya nne.

Habari Zifananazo

Back to top button