RC Manyara aonya utupaji taka ngumu

MANYARA; Babati. Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameonya utupaji wa taka ngumu zinazosababisha kuziba kwa madaraja na mitaro ya maji mkoani humo.

Kutokana na hali hiyo amewaagiza wakurugenzi kusimama usafi wa mitaro ya maji na sehemu za madaraja, ambako wananchi  hutupa taka ngumu zikiwemo chupa za plastiki.

Akizungumza katika kikao cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 cha Bodi ya Barabara kilichofanyika mjini Babati, amesema ni lazima suala hilo lifanyiwe kazi.

Advertisement

“Nimeshuhudia chupa na taka zikizagaa katika mitaro eneo la Korongo Mbili na katikati ya mji, wakurugenzi simamieni hili, usafi ni jukumu la kila mtu,” amesisitiza Sendiga.

Pia amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali mkoani humo kushirikiana na wabunge wa maeneo husika wanapoanzisha miradi mipya ya maendeleo na miradi inayoboreshwa, ili kupata ushauri wa namna bora ya kutekeleza miradi hiyo.

“Kazi za ushirikiano zina tija katika kuondoa migogoro na migongano ya kiutendaji,nendeni site na wapeni taarifa wabunge,” amesema Sendiga.

 

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *