RC Mongella ashangaa chama kipya cha walimu Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema anatambua uwepo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) pekee.
Kutokana na hali hiyo amewaonya baadhi ya maofisa wa Jiji la Arusha wanaopita shule mbalimbali kutangaza kuhusu chama kingine cha walimu.
Mongella ameyasema hayo wakati akizindua miongozo mitatu ya uboreshaji wa elimu Mkoa wa Arusha
Amesema baadhi ya watumishi wa Jiji la Arusha, idara ya elimu wanapita kuhamasisha walimu kujiunga na chama ambacho serikali haikitambui.
Amesisitiza hataki migogoro mkoani kwake na kusisitiza walimu kupendana, ikiwemo maofisa elimu kuacha kupanga safu za waratibu elimu kata au wakuu wa shule, wasiojua maana ya kuchafuka na chaki, kukosa viti au changamoto mbalimbali za walimu