RC Mongella atoa miezi 2 ujenzi wa shule

MKUU wa Mkoa Arusha, John Mongella, ametoa miezi miwili  kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Meru, Zainabu Makwinya kuhakikisha ujenzi wa shule ya Sekondari ya Amsha unakamilika.

Mongella ametoa agizo hilo leo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maji, afya, elimu na miundombinu katika Wilaya ya Meru.

Amesema kabla ya Desemba 14 mwaka huu, shule hiyo Mpya ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo na huduma nyinginezo uwe umekamilika.

Amesema amebaini kuna changamoto ya ukiukwaji wa taratibu za usimamizi wa mradi huo na kumwagiza Mkurugenzi huyo kuhakikisha anatafuta hela nyingine za ziada kwa aajili ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo

“Hapa nimegundua taratibu za usimamizi wa huu mradi zimekiukwa, hata kama shule hii ni shule mama, lakini kwa hili Mkurugenzi hapana sasa tafuta hela iliyobaki mtajua mnatoa kifungu gani nataka madarasa,vyoo,vioo na vitu vingine viwepo hapa, ” amesema.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x