MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa ameipongeza menejimenti ya shule ya Fountain Gate kwa kuwaandaa vizuri vijana wao, wakiwemo wa timu ya wasichana wa mpira wa miguu na kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Shule ya Afrika.
“ Naipongeza timu yetu Fountain Gate kwa kufanya vizuri, lakini wakati mnapita kwenda Dodoma mkawiwa kutusalimu sisi wa Morogoro na hii ni kwa sababu mfugaji bora ni mzaliwa wa Morogoro, mkasema mtupitishie na sisi tuipongeze timu na pia kumpongeza mwana Morogoro na mwalimu anayewafundisha anatokea pia Morogoro, “ amesema Mwassa.
Ameupongeza uongozi wa Fountain Gate kwa kuwa na nia ya kuwekeza shule ya sekondari ya kuinua vipaji mkoani Morogoro na kwamba serikali ya mkoa itatoa ushirikiano kwa kuhakikisha ndoto hiyo inatimia .