RC Mtwara aagiza kusambaratishwa dangulo

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amelazimika kumtuma kamanda wa polisi wa mkoa huo kwenda kusambaratisha dangulo linalohusisha wanafunzi wa shule za sekondari kufanya biashara ya ngono.

Kanali Abbas ametoa agizo hilo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kinachoendelea mkoani hapa baada ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Shule ya sekondari Mkoani (jina linahifahiwa) kulalamika kuhusu dangulo hilo ambalo linatumika kuzorotesha elimu mkoani humu.

“Swala la dangulo,RPC nenda sasa hivi kalisambaratishe ‘immediately.” amesema huku akionyesha kuhuzunishwa na taarifa hizo huku akisema ni fedheha na ukatili mkubwa watoto wa kike na kiume.

Awali akielezea kuhusu dangulo hilo, Mwalimu huyo amesema wasimamizi wa dangulo wanawauza wanafunzi wa kike na wa kiume kutoka Shule mbalimbali za sekondari Mtwara.

“Ukienda pale kuna wamepanga bei tofauti, kuna bei ya wanafunzi wa kike ,unalipia na wanaenda kukuletea mwanafunzi wa kike ,” amesema na kuongeza kuwa “hata ukitaka bei ya Mtoto wa kiume unaletewa,”

Habari Zifananazo

Back to top button