RC Mtwara: Waandishi msiangalie maslahi binafsi

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewataka waandishi wa habari mkoani Mtwara kuacha tabia ya kutanguliza maslahi binafsi pindi wanapokuwa wanatakeleza majukumu yao ya uandishi kupitia kazi za maendeleo ndani ya mkoa.

Pia amewataka maafisa habari mkoani humu kuweka utaratibu mzuri wa kuitangaza miradi yote ya kimkakati na maendeleo ambayo inatekelezwa ndani ya mkoa na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari.

Abbas ametoa wito huo leo Novemba 20, 2023 wakati akizindua jukwaa la Habari na Mawasiliano Mkoa wa Mtwara.

Jukwaa hilo lenye kauli mbiu ya ‘Tumia Vema Kalam una Kamera ya Kulinda Heshima ya Mwanahabari’ limelenga kuwawezesha wanahabari kupata muda wa kujifunza, kujitathimini kupitia kazi ambayo wanaifanya kuhabarisha umma ndani na nje ya Mtwara.

Habari Zifananazo

Back to top button