RC Mwanza asitisha ujenzi jengo la biashara

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amezuia na kusitisha ujenzi wa jengo la biashara katika mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza.

Ujenzi wa jengo hilo kwenye viwanja namba 194 & 195 ulisitishwa rasmi leo. Ujenzi wa jengo hilo ulikuwa chini ya wakandarasi wa kitanzania ambao ni Arch Jse Consult,Savanna engineers, Cost wise consult na Armstrong international.

Akizungumza wakati wa kusimamisha ujenzi wa jengo hilo, Makalla amesema ameamua kuzuia ujenzi wa jengo hilo la biashara ni kutokana na ujenzi viwanja vya jengo hilo ni mali ya serikali na sio eneo la mtu binafsi.

‘’Umilikishaji wa mchakato na ujenzi wa jengo hili ulikuwa ni batili sana na watu wote waliohusika katika katika kughushi viwanja vya jengo hilo walichukuliwa hatua na kamati ya mipango miji ilivunjwa’’ amesema Makalla.

Amesema aliamua kufika katika eneo hilo ili kufuatlia utekelezaji wa agizo la serikali la Julai 20, 2023 lililomtaka anayejenga kusitisha kazi zote kufuatia umilikishaji wake kugubikwa na ukiukwaji wa sheria ya ardhi na taratibu za nchi.

Makalla ameagiza jengo hilo la biashara kuwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na kusiwepo na mtu yoyote kufanya kazi katika jengo hilo.

Amesema uuzwaji wa viwanja hivyo uligubikwa na mizengwe iliyopelekea mgogoro ambapo Serikali iliunda Kamati iliyopendekeza kufanyika kwa taratibu za Urejeshwaji wa hati iliyomilikishwa baada ya kughushi nyaraka za serikali na ujenzi ulisimame.

Amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchin i(TAKUKURU) kusimamia na kuendelea kuchukua hatua kali kwa wahusika ili waweze kufikishwa mahakamani.

Naye msimamizi wa mradi huo wa ujenzi wa jengo la biashara, Emmanuel Kayaya alikiri kupokea barua ya kuzuiliwa kwa ujenzi wa jengo lao tokea Julai 20 mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button