RC Mwanza: Tatueni changamoto kabla ya kunifikia

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amewaagiza wakuu wa wilaya zote saba za mkoa huo kushughulukia matatizo ya wananchi kabla hayajafika katika ofisi yake.

Makalla amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa zoezi malumu la kusikiliza kero za wananchi .

“Wakuu wa wilaya nawataka muwe na utaratibu maalumu wa kuwapa wananchi nafasi ya kutoa kero zao kusikiliza na kufanyia utatuzi.Naomba pia Migogoro ya ardhi itolewe maamuzi mapema kabla haijafika mbali” amesema Makala.

Amesema kabla ya matatizo ya wananchi kufika katika mahakama yapate utatuzi mapema. Amewaagiza wakuu wa Wilaya kupita kata kwa kata kwajili ya kufanya utatuzi wa kero.

Makalla ameahidi kuwa atakuwa anaanda mikutano malumu ya wilaya kwa Wilaya kwajili ya kuweza kutatua matatizo ya wananchi.

Amesema zoezi la usikilizaji wa kero za wananchi litakuwa zoezi endelevu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Kiomoni Kibamba alikanusha uvumi wa kuwa halmashauri yao imeuza soko la kata ya Kirumba.

Amesema Halmashauri yao imetenga Sh bilioni 4 kwa ajili ya kujenga upya soko jipya katika kata ya Kirumba.

Amesema atashirikiana na idara ya ardhi ya manispaa yao kwajili ya kuweza kufanya utatuzi wa kero za ardhi kwa wakati.

  1. Mkazi wa kata ya Luchelele wilayani Nyamagana, Fortunatus Masinde amemuomba mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makalla aweze kuwasaidia utatuzi wa mgogoro wa ardhi wa wakazi 143 katika kata ya Luchelele.

Habari Zifananazo

Back to top button