RC Njombe ashauri wizara tatu kushirikiana teknolojia

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka amezishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Kilimo kushirikiana ili kuendeleza teknolojia zitakazowezesha kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Ushauri huo ameutoa alipotembelea banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) katika maonesho ya nane nane yanayoendelea mkoani Mbeya.

Amesema kwa wizara hizo kushirikiana itaongeza tija kwa kuwa serikali inaendelea kuuwisha tume hiyo iweze kuendeleza tafiti na bunifu zinazofanywa na vijana katika maeneo mbalimbali nchini.

Pia amepongeza tume hiyo kwa kubeba dhana ya Kilimo Biashara kwa kuwa ni taasisi inayosaidia watafiti na wabunifu.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button