RC Shigela asisitiza maadili ya kidini kwa watoto

MKUU wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amewataka wazazi na walezi mkoani hapa kuwekeza zaidi katika maadili ya kidini kwa watoto ili waweze kukua katika njia sahihi ya kufikia ndoto zao.

Shigella amesema hayo Desemba 23, 2022 mara baada ya kukabidhi zawadi ya Rais Samia Suluhu kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto kutoka mazingira magumu cha Moyo wa Huruma mjini Geita.

Amesema msingi ya kidini inasaidia watoto wote ikiwemo watoto wanaolelewa kwenye vituo kuishi kwa usalama wa kimwili na kisaikolojia na baadaye kuwa na tija kwa taifa.

Shigella amewaomba watoto wanaolelewa kituoni hapo kusoma kwa bidii kwani serikali ya Rais Samia inapambana kuweka mazingira rafiki ya kielimu kwa kila mtoto bila kujali uchumi wake.

“Nimetumwa kuwapatia zawadi hizi ikiwemo mbuzi wanne, mchele kilo 200, mafuta, maharage, na viungo vya mboga pamoja na vinywaji ili muweze kusherehekea krismasi kwa amani zaidi.”

Akisoma risala ya kituo cha Moyo wa Huruma, Joseph Francis amesema tangu mwaka 2006 hadi 2022 kituo kimelea jumla ya watoto 179 kati yao 17 wamesharudishwa kwa ndugu tayari.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x