MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika kutoa huduma za kijamii na kiroho ikiwemo kudumisha amani.
Mndeme aliyasema hayo Jana wakati akiwa mgeni rasmi katika sherehe za kumuweka wakfu Askofu wa kanisa la KKKT wa Dayosisi ya kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Dk Yohana Nzelu.
Mdeme aliwataka wananchi kufuata maadili na sio kufuata mila za kigeni na kuwataka waishi katika amri kumi za mungu na watoto waendelee kufundishwa.
“Nimeanzisha kampeni ya usiniguse yaani ‘Don’t touch me ‘ katika utawala wangu nakuwaeleza watoto wasikubali kufanyiwa vitendo viovu watoe taarifa na vikemewe kwa nguvu zote”alisema Mndeme.
Mndeme alisema wataendelea kushirikiana na Askofu aliyeteuliwa Kama ilivyokuwa yule aliyestaafu Emanuel Makala alikuwa mwenyekiti wa amani wa mkoa.
Mndeme alisema changamoto zilizoelezwa na Askofu Nzelu zinafanyiwa kazi kwani kwa Kahama barabara ya kutoka Kakola kwenda