MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amewataka wataalamu na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato kwani kuanzia Julai 2022 hadi Juni 19, 2023 wamefikia asilimia 75 ya ukusanyaji .
Mndeme alisema hayo Jana kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujibu hoja za mkaguzia ambapo alisema bado asilimia 25 ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji mapato kwa mwaka.
Mndeme alisema hoja ambazo hazijafungwa mojawapo ni magari kumi na moja kutokatiwa bima, zaidi ya Sh milioni 850 kudai kwa wadaiwa mbalimbali na kutopelekwa Fedha Kwenye mfuko wa PSSF Sh milion 162.
“Nimesikia hoja 76 mlikuwa nazo na hoja 13 zimefungwa bado hoja 64 hamjajibu hivyo hoja hizi ni nyingi ni halmashauri ya mwisho ndani ya mkoa huu kuwa na hoja nyingi ninawashauri mkienda hivi mtatangazwa kitaifa kuwa wa mwisho” alisema Mndeme.
Mndeme alisikitishwa na taarifa ya kutaka kushusha ushuru wa karasha kutoka Sh 120,000 hadi kufikia Sh 50,000 hilo bado halijaafikiwa aliitaka halmashauri kutathimini kushusha huko Kama utaleta tija kwani mapato yanatakiwa yapande.
“Halmashauri hii inatakiwa isimamie sheria,kanuni na miongozo kwani nafahamu mnaweza ipo timu nzuri ya wataalamu na madiwani ndiyo maana mmepata hati safi kazi iendelee nakujipanga kwenye ukaguzi wa mwaka ujao” alisema Mndeme.
Mkaguzi Mkuu wa Hsabau za Serikali Mkoa wa Shinyanga, Patrick Lugisi ameshauri kamati ya fedha iwe inaandaa taarifa za muhtasari wa kikao hivyo vizuri ili kurahisisha wakaguzi na iwe rahisi kwao kujibu hoja.
“Halmashauri hii inahoja 56 ambazo bado hazijajibiwa zinatakiwa kufanyiwa kazi ili isibaki hata hoja moja nitakuwa namkumbusha katibu Tawala kuhusu suala la kuondoa hoja”alisema Lugisi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Edward Ngelela aliwata wataalamu na madiwani kuendelea kujibu hoja kwani zipo ambazo zinaweza kujibika na kufungwa hoja zikiwa nyingi kunakuwana mashaka pia.
Comments are closed.