RC Tanga aeleza kilichomponza DED Muheza

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omar Mgumba ametaja sababu za kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Nasib Mbaga kuwa ni kutoheshimu maamuzi ya vikao pamoja na kutoshiriki vikao vya Baraza la Madiwani.

Hayo ameyasema wakati wa kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amesema kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa akishindwa kushiriki vikao na badala yake anatuma wawakikishi.

“Hatuwezi kufanya kazi kwa mtindo huo wa kutuma wawakilishi kisha kubadilisha maamuzi ya vikao vya kisheria ambavyo wewe [mkurugenzi] kama mtendaji umeshindwa kuhudhuria,” amesema RC Mgumba

Mkurungenzi wa Muheza amesimamishwa kazi mnamo Agosti 30 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Innocent Bashungwa kutoka na kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Habari Zifananazo

Back to top button