RC Tanga amaliza mgogoro wa mipaka

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amemaliza mgogoro wa mpaka kati ya kijiji cha Gitu na Ngobore uliodumu kwa miaka 17 kutoka na vijiji hivyo kugombea vitongoji vya Komtindi na Ngoloji vilivyopo Wilaya Kilindi.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Gitu RC Kindamba amesema kuwa vitongoji hivyo kwa sasa vitakuwa chini ya kijiji cha Gitu kutokana na alama ya mpaka (GN) kuonyesha kuwa kipo katika eneo hilo.

“Huu mgogoro Sasa umekwisha vitongoji hivyo Sasa vipo chini ya Gitu nasio Ngobore kama ambavyo mlivyokuwa mnagombea maeneo ya ardhi na kusababisha vurugu”amesema RC Kindamba.

Aidha ametoa eneo la zaidi ya hekta 2000 zilizopo mpaka mwa kijiji cha Ngobore kilichopo kata ya Saunyi na kijiji cha Gitu kilichopo kata ya Kibirashi kuwa mali ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT.

Mgogoro huo wa ardhi ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 17 umefikia ukomo wake baada ya Rais Samia Suluhu kumuagiza Mkuu wa mkoa wa Tanga kuutatuw mgogoro huo.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button