RC Tanga aonya viongozi mamlaka yasiyowahusu

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amepiga marufuku wanasiasa na viongozi kuacha kuwachukulia hatua za kinidhamu wauguzi, bali waviache vyombo vya kitaaluma kufanya hivyo.

Maelekezo hayo ameyatoa jana wakati wa maadhimisho ya uuguzi na ukunga ambapo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Mkinga amesema kuwa tayari sekta hiyo inavyombo vyake vya kusimamia maadili yao.

Amewataka wanasiasa kuheshimu kada hiyo na kuacha kuwaingilia katika maamuzi yanayohusu taaluma hiyo kwani Kwa kufanya hivyo wanasababisha kuzorotesha huduma za afya Kwa wananchi.

Advertisement

“Sitarijii kusikia Mkuu wa Wilaya kamuweka ndani muuguzi au mtumishi wa afya kutokana na utovu wa nidhamu bali natarajia busara na hekima itawale pale ambapo Kuna changamoto za kinidhamu basi wazihusishe Bodi zao za kitaaluma katika kufanya maamuzi

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Rehema Maggid alisema kuwa tayari Serikali imeanza kushughulikia changamoto ya uhaba wa watumishi katika kada hiyo kwa kuajiri wapya 527 ambao watasambazwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Mkoa wa Tanga, Abeid Njopa amesema kuwa maadhimisho hayo yanalengo la kueleza mafanikio waliyoyapata katika kipindi Cha mwaka mmoja na changamoto ambazo waliweza kuzipitia

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *