RC Tanga ataka mikakati kupunguza udumavu

RC Tanga ataka mikakati kupunguza udumavu

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba ameziagiza halmashauri kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa àjili ya kutekeleza afua za lishe zinatekeleza miradi husika, ili kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Hayo ameyasema wakati akifungua kikao cha utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Juni 2022.

Amesema kuwa sababu halmashauri kutokufanya vizuri katika utekelezaji wa mpango huo ni kutokana na changamoto ya uwepo wa bajeti finyu, licha ya serikali kutoa miongozo ya kuwepo na fedha.

Advertisement

“Tanga hali ya udumavu ipo juu zaidi ya asilimia 34, lakini bado tunashindwa kutekeleza afua za lishe ipasavyo, ili kumaliza changamoto hiyo,” amesema RC Mgumba.

Ofisa lishe mkoa, Mwamvua Zuber amesema kuwa zaidi ya asilimia 35 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano mkoani humo vinasabashwa na lishe duni.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Jonathan Budenu, amesema kuwa tayari mkoa una vituo viwili vya kuhudumia watoto wenye udumavu.