RC Tanga atangaza fursa za Utalii

TANGA; Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dk Batilda Burian amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Tanga umeweza kupokea fedha ambazo zimetumika katika kurekebisha miundombinu hasa upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo inaenda kufungua fursa za uwekezaji katika mikoa ya kaskazini.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 11 ya biashara na utalii Tanga yajulikanayo Tanga trade fair ambayo yanafanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya usagara Jijini Tanga

Amesema Bandari ya Tanga imeboreshwa na inauwezo kwa kupokea shehena nyingi zaidi za mizigo na siku za kutoa mizigo ni tatu pekee na sio zaidi hapo lakini na  huduma zote muhimu zinapatikana katika eneo moja kwa hiyo shughuli imekuwa rahisi.

Advertisement

“Mkoa wa Tanga utaendelea kufungua na kurasimisha bandari nyingine ndogo zilizokuwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya  ili kurahisha kazi za bandari ikiwemo kudhibiti bidhaa za magendo “amesema mkuu wa mkoa

Katika upande wa barabara Dk Batilda amesema ujenzi wa barabara ya Tanga, Pangani, Saadani hadi Bagamoyo itafungua fursa ya utalii katika ukanda wa kaskazini.

Nae Rais wa Chemba ya biashara na uchumi nchini TCCIA Vincent Minja amesema kuwa maonesho hayo yameweza kuibua fursa za kimaendeleo zilizopo hivyo kuitaka serikali ya mkoa huo kuendelea kutoa kipaumbele cha uwepo wa maonesho hayo kila mwaka.