RC Tanga atoa maagizo taa za barabarani

TANGA; Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk Batlida Burian ametoa wiki tatu kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga, kuhakikisha taa za barabara zinawaka, ili kutoa fursa kwa wajasiriamali na wananchi kufanya biashara zao hata nyakati za usiku.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea hali ya uwakaji wa taa hizo, Dk Burian ameitaka Halmashauri ya Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka, ili taa zote ambazo hazifanyi kazi kuhakikisha zinarekebishwa.

Amesema karibu taa 600 zilizounganishwa na Tanesco hazifanyi kazi na wamekubaliana na jiji kuzifanyia marekebisho, ili zirejee katika hali yake ya kawaida, wakati wakisubiri uunganishwaji wa taa zinazotumia sola.

Amesema uwakaji wa taa za barabarani katika mitaa kutachagiza maendeleo ya wananchi wa Jiji la Tanga, sambamba na kuimarisha usalama wakati wakifanya shughuli zao.

Habari Zifananazo

Back to top button