‘REA haitatoa kazi kwa wakandarasi wababaishaji’
MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, amesema serikali haitatoa kazi kwa mkandarasi yeyote ambaye anafanya kazi chini ya kiwango au analeta usumbufu kwenye utekelezaji wa miradi ya wakala huo nchini.
Amesema hatua hizo zitakwenda sambamba na uondoaji wa sifa za kuendelea kupewa miradi kwa wakandarasi ambao wana viporo kwenye utekelezaji wa miradi ya REA II.
“Mtu (Mkandarasi) yeyote ambaye ana viporo kwenye REA II huyu automatically anakuwa disqualified,” amesema.
Hatua hiyo itawahusisha pia wakandarasi ambao wanaotekeleza miradi ya REA III, ambapo amesema kwa mkandarasi ambaye mpaka sasa hajakamilisha asilimia 60 ya utekelezaji wa mradi hiyo ya REA III hatua ya kwanza kwanza na wataondolewa sifa ya kuendelea kuaminiwa na kupewa miradi kwenye miradi mingine.
Amesema wakandarasi hao hawatahusishwa tena kwenye miikataba itakayokuja baada ya huu wa REA III hatua ya kwanza
Saidy ametoa kauli hiyo wakati wa kikao baina ya watendaji wa REA Mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa, wakandarasi pamoja ana wabunge kuhusu utekelezaji wa miradi ya REA Mkoani humu.
Mapema akifunguo kikao hicho, Kanali Abbas ameeleza kutoridhishwa na utekelezaji wa watendaji wa REA hatua ambayo amesema imekuwa inaleta sintofahamu kwa serikali na chama tawala.