REA wazindua mradi wa Sh Bil 11 Mtwara

MRADI wa kusambaza Umeme kwenye maeneo yenye sifa za Vijiji na pembezoni mwa Miji, Majiji ulio chini ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu umezinduliwa rasmi leo mkoani Mtwara na utagharimu Shilingi Bilioni 11.25.

Akizumza leo mkoani Mtwara, Mkurugenzi wa Fedha na Uhamasishaji Rasilimali Fedha REA Makao Makuu, Daniel Mungure,  amesema mradi huo ni wa miezi 18 na utaanza kutekelezwa Januari mwaka huu kwenye wilaya tatu mkoani humo, ikiwemo Manispaa ya Mtwara Mikindani, Newala pamoja  wa Masasi.

Katika mradi huo Wateja wa awali 2,229 wataunganishiwa  umeme na utapita kwenye maeneo 40 mkoani humo na kilomita za mfumo wa umeme ni  75.6 na kilomita 149.2 ni za mfumo wa umeme mdogo  zitajengwa kwenye wilaya hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abas amewataka watekelezaji wa mradi huo kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa, lakini pia watambue kukamilika kwa kazi zao hizo ndizo zinazoenda kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Amesema Mkoa wa Mtwara  ni sehemu ya wanufaika wa mradi huo kati ya Mikoa nane inayonufaika na mradi nchini hivyo kutokana mradi unatekelezwa na fedha nyingi, matarajio yao ni kuona thamani ya fedha inaendana na kazi husika.

“Bilioni 11.25 si fedha ndogo ni fedha nyingi kwa hiyo tunatarajia kuona thamani ya fedha iendane na kazi inayofanyika pia tunatarajia kuona muda wa kutekelezwa mradi uwe ndani ya hiyo miezi 18 au chini ya mda huo, ili mradi umalizike na uanze kutumika”,amesema Abas .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Kanda ya Kusini, Mhandisi Maganza Mashala amesisitia suala la kukamilishwa kwa mradi huo kwa wakati ndani ya miezi hiyo au chini ya hapo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button