REA yaita wanaotaka kufungua vituo vya mafuta vijijini

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA),  imewaita wananchi wenye nia ya kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini kufika katika banda lao kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), ili kuelekezwa namna ya kutuma maombi ya mkopo wa fedha kwa ajili ya ujenzi huo.

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi REA, Jones Olotu amesema hayo katika banda lao lililopo kwenye maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere Da es Salaam.

Amesema hiyo ni fursa kwa wananchi, hivyo wajitokeze kuwekeza kwenye eneo hilo ambalo kimsingi REA imelenga kuboresha hali ya wananchi hususani waishio kijijini.

“Watumie maonesho haya waweze kujifunza namna ya kukopa na kujua kiwango cha riba cha mkopo atakaochukua na namna ya urejeshaji,” amesema Olotu.

“Vituo hivyo vitaokoa usalama wa waendesha pikipiki vijijini kulala na petroli nyumbani kwa kuyaweka kwenye madumu kwa sababu ya ukosefu wa vituo vya mafuta karibu na maeneo ya vijiji vyao,” amesema Olotu na kuongeza kuwa hiyo ni fursa ya wazi kwa wenye vigezo.

Kuhusu miradi inayotekelezwa na REA amesema inalenga kuinua maisha ya Mtanzania, ikiwamo ile ya nishati safi ya kupitia itakayomuondoa mama kwenye maisha ya machozi kwa kupikia kuni zenye moshi.

Amesema mradi huo pia unatarajiwa kupunguza kiwango cha  watu wanaokufa kila mwaka kutokana na moshi wa kupikia kutoka watu 33,000 kwa mwaka na kushuka.

Kwa upande wa mjumbe wa Bodi ya REA, Francis Songela amesema wakala huo una miradi ya kupeleka vijiji vyote nchini, hatua ambayo itaibua fursa mbalimbali zitokanazo na nishati hiyo.

Amesema umeme unafungua fursa nyingi za uwekezaji, kwa watu wa vijijini itakuwa na manufaa makubwa na kukuza uchumi pia.

 

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button