Real Madrid yamtetea Zidane

MABINGWA wa kihistoria wa Ulaya Real Madrid wamesikitishwa na kauli isiyo ya kiungwana na iliyotafisiriwa kumkosea heshima ya Rais wa Shirikisho la soka la Ufaransa, Noel Le Graet, kumhusu Zinedine Zidane.

Baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ziliibuka tetesi kuwa kiungo wa zamani wa Real Madrid na Ufaransa, Zinedine Zidane kuwa angeweza kuwa kocha wa Ufaransa au Brazil.

Tetesi za kuhusishwa na kuifundisha Brazil, Rais Noel Le Graet hakupendezeshwa nayo na aliposikia taarifa hizo alisema  “𝒁𝒊𝒅𝒂𝒏𝒆 𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒌𝒐𝒄𝒉𝒂 𝒘𝒂 𝑩𝒓𝒂𝒛𝒊𝒍? 𝑯𝒂𝒊𝒏𝒊𝒔𝒕𝒖𝒊 𝒉𝒂𝒕𝒂 𝒌𝒊𝒅𝒐𝒈𝒐, 𝒂𝒏𝒂𝒘𝒆𝒛𝒂 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒅𝒂 𝒌𝒐𝒌𝒐𝒕𝒆 𝒂𝒏𝒂𝒌𝒐𝒕𝒂𝒌𝒂! 𝑰𝒘𝒆 𝒏𝒈𝒂𝒛𝒊 𝒚𝒂 𝒌𝒍𝒂𝒃𝒖 𝒂𝒖 𝒏𝒈𝒂𝒛𝒊 𝒚𝒂 𝒕𝒊𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒕𝒂𝒊𝒇𝒂, 𝒔𝒊𝒂𝒎𝒊𝒏𝒊 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒄𝒉𝒐𝒄𝒉𝒐𝒕𝒆 𝒌𝒊𝒏𝒂𝒄𝒉𝒐𝒏𝒕𝒊𝒂 𝒔𝒉𝒂𝒌𝒂.

“𝑨𝒍𝒊𝒘𝒂𝒉𝒊 𝒌𝒖𝒘𝒂𝒔𝒊𝒍𝒊𝒂𝒏𝒂 𝒏𝒂 𝒎𝒊𝒎𝒊 𝒂𝒘𝒆 𝒌𝒐𝒄𝒉𝒂 𝒘𝒂 𝒕𝒊𝒎𝒖 𝒚𝒂 𝒕𝒂𝒊𝒇𝒂? 𝑯𝒂𝒑𝒂𝒏𝒂, 𝒏𝒂 𝒏𝒊𝒔𝒊𝒏𝒈𝒆𝒑𝒐𝒌𝒆𝒂 𝒉𝒂𝒕𝒂 𝒔𝒊𝒎𝒖 𝒚𝒂𝒌𝒆.” aliongeza

Katika taarifa yao Real Madrid wameandika.

“Zinedine Zidane, bingwa wa dunia na bingwa wa Ulaya akipigania jezi ya taifa lake, pamoja na mataji mengine mengi, anawakilisha tunu za mchezo huu na amethibitisha hilo katika maisha yake yote ya soka, kama mchezaji na kama kocha.”

“Kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Ufaransa haikubaliki hasa kwa mtu anayebeba uwakilishi kama wake, na inamdhalilisha mwenyewe, ukirejea pia alishawahi kutoa kauli kama hizo kwa nahodha wetu Karim Benzema, mshindi wa sasa wa Ballon d’Or, Ligi ya mataifa ya Ulaya akiwa na Ufaransa mwaka 2021 na mshindi mara tano wa ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na mataji mengine mengi.”

Habari Zifananazo

Back to top button