Redio za Taifa kusikika Loliondo, Kyela, Makete na Mbinga

LOLIONDO, Arusha: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko leo tarehe 15 Aprili, 2024 amezindua vituo vya kurushia matangazo ya Redio vya Shirika la Utangazaji nchini, TBC Taifa na Bongo FM.

Uzinduzi huo umefanyika Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa niaba ya vituo vingine vya Uvinza, Kyela, Makete na Mbinga.

Viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya Habari na Mawasiliano wamehudhuria akiwemo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Habari Zifananazo

Back to top button