Reece James aomba radhi

BEKI wa Chelsea, Reece James ameomba radhi kwa makosa mawili aliyofanya na kupelekea kupewa kadi nyekundu katika mchezo waliopoteza mabao 4-1 dhidi ya New Castle United jana.


James alipewa kadi ya njano dakika ya 55 kwa kupinga maamuzi ya mwamuzi na kupiga mpira, baadaye alipewa tena njano na kuwa nyekundu kwa kumsukuma winga Anthony Gordon na hivyo atakosa mechi moja.

“Somo lingine la kujifunza, naomba radhi kwa mashabiki na wachezaji wenzangu tulikuwa chini ya viwango vyetu lakini mchezo huu hautufafanui.” amesema James.

Mchezo ujao wa EPL, Chelsea atakuwa nyumbani uwanja wa darajani kuwakaribisha Brighton.

Advertisement
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *