Ripoti CAG kujadiliwa Novemba

SPIKA wa Bunge, Tulia Ackson amesema kwa sasa serikali haitalazimika kujibu chochote kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hadi mwezi Novemba baada ya Kamati za PAC na LAAC kuwapa nafasi watuhumiwa kujitetea.

Spika ametoa kauli hiyo Alhamisi Aprili 13, 2023 wakati akitolea ufafanuzi juu ya michango ya wabunge kuhurusu ripoti hiyo ambayo mara kadhaa imeleta sintofahamu ndani ya bunge kwenye michango ya baadhi ya wabunge.

Aidha, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameruhusu wabunge na Watanzania kuijadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa namna wanavyoona wako sahihi.

Spika amesema kwa kuwa ripoti imeshawasilishwa mbele ya bunge, ni haki kuijadili na akazuia wabunge wenye utaratibu wa kusimama na kuwapa taarifa wabunge wenzao wanaochangia kwenye Ripoti ya CAG kuacha mara moja.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button