Robertinho: Hakuna wa kulaumiwa

BAADA ya kikosi cha Simba, kurejea nchini kikitokea nchini Morocco ambako juzi kilitolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Wydad Casablanca, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Roberto Oloveira ‘Robertinho’ amesema anajivunia kiwango bora kilichooneshwa na wachezaji wake na hawezi kumlaumu mtu kwa kukosa penalti.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa kwa walichokionesha kwenye mchezo huo kimedhihirisha ubora wa soka la Tanzania lakini pia ukubwa wa Simba na sasa duniani kote timu hiyo imekuwa gumzo na tishio.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kujitoa kuipigania timu yao naamini tulikosa bahati lakini tulifanya kila kilichotakiwa ndani ya uwanja, tumekubali matokeo tumerudi nyumbani na tunajipanga kwa ajili ya mechi za mashindano ya ndani ambazo zinatukabili lengo likiwa ni kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Robertinh

Juzi Simba iliondoshwa kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika, kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini kila mmoja akishinda bao 1 kwenye uwanja wa nyumbani.

Habari Zifananazo

Back to top button